Atupele Green.
MSHAMBULIAJI wa Ndanda FC, Atupele
Green, ameamua kulipa mkono wa kwaheri soka la Bongo baada ya kusema kuwa msimu ujao hatarajii kuwepo katika Ligi Kuu Tanzania Bara.
Alisema mipango yake ni kucheza soka la kulipwa na sasa yupo kwenye harakati za kumalizia mipango yake na kama ikienda sawa msimu ujao hatakuwepa nchini.
“Kwa sasa siwezi kusema ninakwenda kucheza wapi lakini ukae ukijua kuwa kuna uwezekano mkubwa sana msimu ujao nikacheza soka la kulipwa kwani zipo zaidi ya timu moja kutoka nchi mbalimbali zinazohitaji huduma yangu,” alisema.
Alisema umefika wakati kwenda kujaribu soka la kulipwa na anamuomba Mungu harakati zake hizo za kwenda nje ya nchi
zikamilike bila kikwazo chochote.
Licha ya kwamba, straika huyo ameshindwa kuweka bayana nchi anayotarajia kutimkia,lakini kuna taarifa kuwa Zesco ya Zambia inamuwinda huku pia Dongtan Longan ya Malaysia nayo ikitajwa kumwahidi donge nono.
CHANZO:BINGWA
0 comments:
Post a Comment