728x90 AdSpace

Sunday, April 10, 2016

MANNY PACQUIAO ACHAPA MTU KWA POINTI

Las Vegas, Marekani.

Manny Pacquiao ameonyesha umwamba kwa kumtwanga bondia Mmarekani, Timothy
Bradley kwa pointi alfajiri ya leo.

Katika pambano hilo lililofanyika kwenye Ukumbi maarufu wa MGM Grand jijini Las Vegas, Marekani, Pacquiao alimwangusha chini Bradley mara mbili katika raundi ya saba na tisa na kuwafanya majaji wote watatu wampe ushindi wa pointi.

Katika mpambano huo Pacquiao alimchapa Bradley makonde 122 huku yeye akichapwa makonde 99 pekee.





  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Post a Comment

Item Reviewed: MANNY PACQUIAO ACHAPA MTU KWA POINTI Rating: 5 Reviewed By: Unknown