Bourdeax, Ufaransa.
Ujerumani imevunja mwiko wa kutokuifunga Italia katika michuano mikubwa baada ya usiku huu kushinda kwa penati 6-5 kufuatia sare ya bao 1-1 ndani ya dakika 120 katika mchezo mkali wa robo fainali uliochezwa katika uwanja wa Nouveau Stade de Bordeaux huko Bordeaux.
Mesut Ozil alianza kuifungia bao la kuongoza Ujerumani akiunganisha krosi ya Jonas Hector,Italia wakasawazisha kupitia mkwaju wa penati wa Leonardo Bonucci na kuufanya mchezo uishe kwa sare ya bao 1-1.
Hali iliyomlazimu mwamuzi Victor Kassai kutoa Hungary kuamuru zipigwe penati na Ujerumani kufanikiwa kuibuka washindi.
Kwa matokeo hayo Ujerumani itacheza nusu fainali dhidi ya mshindi wa mchezo wa kesho Jumapili kati ya wenyeji Ufaransa na Iceland.
VIKOSI
Germany: Neuer; Hector, Höwedes, Hummels,Khedira, Özil, Müller, Boateng, Kroos, Kimmich,Gomez
Italy: Buffon, Barzagli, Bonucci, Chiellini;
Florenzi, Parolo, Sturaro, Giaccherini, De
Sciglio, Pelle, Eder
0 comments:
Post a Comment