Pretoria, Afrika Kusini.
Mamelodi Sundowns imekuwa timu ya kwanza kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya klabu bingwa Afrika baada ya Jumatano usiku kuchomoza na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Zamalek ya Misri katika mchezo mkali wa kundi B uliochezwa katika uwanja wa Lucas Moripe Stadium,Atteridgeville,Pretoria (Afrika Kusini)
Bao lililoipa ushindi huo wa kihistoria Mamelodi Sundowns limepatikana dakika ya 79 baada ya mlinzi wa Zamalek,Ali Gabr Mossad,kujifunga akiwa katika harakati za kuokoa krosi ya Percy Tau toka winga ya kushoto na kufanya wenyeji watinge nusu fainali wakiwa na mchezo mmoja mkononi.
Kwa matokeo hayo sasa Zamalek inahitaji kushinda ama kutoka sare yoyote ile dhidi ya Enyimba hapo Agosti 13 katika mchezo wake wa mwisho ili iweze kuungana na Mamelodi Sundowns katika hatua ya nusu fainali.
VIKOSI
Mamelodi Sundowns: Onyango; S.Zwane,Nthethe, Bangaly,Langerman – Kekana,Modise (Mbekile 86′), T.Zwane (Tau 65′) –Dolly, Billiat, Castro
Zamalek: El-Shenawy; Ali Fathy, Dowidar,Gabr, Tolba (Fathi 81′) – Tawfix,Youssef,Abdelkhalik – Shikabala (Abdelkader 69′),Khaled (Hefny 83′), Morsy
0 comments:
Post a Comment