London,England.
LEO Alhamis Chama cha soka cha England (FA) kinatarajia kumtangaza Kocha wa Sunderland,Sam Allardyce,kuwa kocha mpya wa timu ya soka ya taifa hilo akichukua nafasi iliyoachwa wazi na kocha Roy Hodgson aliyemaliza mkataba wake.
Mtendaji Mkuu wa FA, Martin Glenn,ametanabaisha kuwa Bodi ya watu 12 ya FA itajulishwa rasmi kuhusu mchakato wa uteuzi wa kocha wa timu ya taifa ili itoe uamuzi katika Kikao chao cha leo Alhamis.
Allardyce mwenye umri wa miaka 61 sasa amepata fursa hiyo baada ya kumbwaga mpinzani wake Steve Bruce anayeifundisha Hull City iliyopanda daraja na kurejea Ligi Kuu England.
Mchakato wa kumpata mrithi wa Roy Hodgson uliwekwa mikononi mwa jopo lililokuwa chini ya Martin Glenn (Mwenyekiti),David Gill (Makamu Mwenyekiti) na Dan Ashworth (Mkurugenzi wa ufundi)
Uteuzi huo wa Allardyce ni ushindi kwa kocha wa zamani wa Man United,Sir Alex Ferguson,ambaye mapema mwezi uliopita aliwaeleza wazi viongozi wa FA kuwa mtu pekee anayefaa kuwa Kocha wa England kwa sasa ni Sam Allardyce maarufu kama BIG SAM.
0 comments:
Post a Comment