728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, July 21, 2016

    MAN UNITED YAKUBALI KUMSAJILI PAUL POGBA KWA DAU LA REKODI YA DUNIA

    Manchester,England.

    TAARIFA kutoka vyombo mbalimbali vya habari vya kimataifa zinasema klabu ya Manchester United imekubali kutoa dau la rekodi la £100m ili kumsajili kiungo wake wa zamani,Paul Labile Pogba,ambaye kwasasa anachezea Juventus.

    Makubaliano ya dili hilo yamefikisha Jumatano usiku kufuatia mwenyeji wa Manchester United,Ed Woodward,kufanya mazungumzo mazito na Wakurugenzi wa Juventus,Giuseppe Marotta na Fabio Paratici,pamoja na Wakala wa Pogba anayeitwa Mino Raiola.

    Taarifa zaidi zinasema ikiwa kila kitu kitakwenda sawa Pogba mwenye umri wa miaka 23 atasaini mkataba mnono wa miaka mitano utakaomwezesha kuvuna mshahara wa £210,000 kwa wiki na kuwa mmoja kati ya nyota wanaolipwa vizuri England.

    Pogba aliiacha Manchester United mwaka 2012 na kutimkia Juventus akiwa mchezaji huru baada ya kushindwa kupata namba katika kikosi cha kwanza ambacho wakati huo kilikuwa chini Sir Alex Ferguson.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MAN UNITED YAKUBALI KUMSAJILI PAUL POGBA KWA DAU LA REKODI YA DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top