Genk,Ubelgiji.
KLABU ya KRC Genk inayochezewa na Mshambuliaji wa Kimataifa wa Tanzania,Mbwana Samatta,imefanikiwa kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Cork City FC ya Ireland katika mchezo
wa kwanza wa Raundi ya Tatu ya mchujo wa kuwania kuingia hatua ya
makundi yamichuano ya Europa League uliofanyika katika uwanja wa Luminus Stadium,Genk.
Bao lililoipa ushindi huo KRC Genk limefungwa na Mjamaica,Leon
Bailey,dakika ya 31 ya mchezo kwa shuti hafifu la mguu wa kushoto lililomshinda kipa wa Cork City,Mark McNulty,na kutinga wavuni.
Kwa matokeo hayo KRC Genk watatakiwa kushinda ama kutoka sare yoyote ile katika mchezo wao wa marudiano utakaochezwa Agosti 4,2016 huko nchini Ireland.
Katika mchezo huo ambao Samatta alicheza dakika zote tisini KRC Genk ilikifanyia mabadiliko matatu kikosi chake cha kwanza.Sandy
Walsh alianza badala ya majeruhi Timothy Castagne,Dries Wouters alichukua nafasi ya Bennard Kumordzi aliyefungiwa huku kiungo wake Mhispania,Alejandro Pozuelo,akianza badala ya Yoni Buyens.
VIKOSI
KRC Genk: Marco Bizot; Sandy Walsh,Sébastien Dewaest, Dries Wouters, Jere Uronen; Wilfred Ndidi; Thomas Buffel,Alejandro Pozuelo (Brian Heynen '82), Ally Samatta, Leon Bailey; Nikolaos Karelis (Neeskens Kebano '72).
Cork City: Mark McNulty; Michael McSweeney, Alan Bennett, Kenny Browne,Kevin O'Connor; Steven Beattie (Danny Morrissey '83), Garry Buckley, Greg Bolger,Gearoid Morrissey, Stephen Dooley; Sean Maguire (Mark O'Sullivan '86).
Mwamuzi:Clayton Pisani (Malta)
0 comments:
Post a Comment