728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, July 29, 2016

    DEWJI AAHIDI NEEMA KUBWA SIMBA,SASA KAZI KWENU WANACHAMA

    Dar es Salaam,Tanzania.

    MFANYABIASHARA maarufu nchini,Mohammed Gulam Dewji ama 'MO' amefunguka hadharani na kutamka kuwa yupo tayari kufanya uwekezaji wa bilioni 20 kwa klabu ya Simba endapo tu wanachama wa klabu hiyo kongwe nchini wataridhia mpango wake huo.

    Mo amekuwa akihusishwa na kutaka kufanya uwekezaji huo mkubwa ndani ya Simba huku baadhi ya wanachama wa
    klabu hiyo wakionekana kutokuwa tayari kutokana na sababu zao binafsi.

    Akizungumza na waandishi wa habari ofisi kwake jijini Dar es Salaam leo asubuhi,MO amesema kinachomvutia kufanya uwekezaji huo
    mkubwa kwa Simba ni mapenzi aliyonayo kwa klabu hiyo.

     "Naipenda Simba toka moyoni,niliwahi kuidhamini miaka ya nyuma na tulifanya vizuri sana katika michuano ya kimataifa kila Mwanasimba analijua," amesema MO.

    Wakati huohuo Mo amesema bajeti ndogo ya Simba ndiyo inayoifanya klabu hiyo kushindwa kushindana vizuri katika soko la usajili na vilabu vya Yanga na Azam.

    Mo ameongeza kuwa endapo atapewa ridhaa ya kufanya uwekezaji basi ndani ya miaka mitatu ataijengea klabu hiyo kiwanja bora cha mpira,hosteli, Gym na kuajiri makocha mwenye vigezo.

    Simba inatarajiwa kufanya mkutano mkuu wa wanachama utakaojadili juu ya uwendeshwaji wa klabu hiyo siku ya Jumapili katika Bwalo la Maofisa wa Polisi.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: DEWJI AAHIDI NEEMA KUBWA SIMBA,SASA KAZI KWENU WANACHAMA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top