Munich,Ujerumani.
Pep Guardiola ameanza kichwa chini safari yake ya kukinoa kikosi cha Manchester City baada ya Jumatano Usiku kukishuhudia kikosi hicho kilichokuwa na chipukizi wengi kikichapwa bao 1-0 na klabu yake ya zamani ya Bayern Munich katika mchezo mkali wa kimataifa wa kirafiki uliochezwa katika uwanja wa Allianz Arena huko Munich,Ujerumani.
Bao pekee la mchezo huo uliotawaliwa kwa kiasi kikubwa na Bayern Munich limefungwa dakika ya 76 na Erdal Ozturk.
Guardiola na Manchester City yake watarejea tena dimbani huko China siku ya Jumatatu pale watakapovaana na Manchester United katika michuano ya kimataifa ya Champions Cup.
0 comments:
Post a Comment