728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, July 28, 2016

    KOCHA SIMBA AIPA POLE YANGA,AELEZA KILICHOIUA SHIRIKISHO

    Morogoro,Tanzania.

    KOCHA msaidizi wa Simba, Jackson Mayanja amewapa pole wapinzani
    wao Yanga kutokana na matokeo mabaya wanayoyapata kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, hatua ya makundi na kuwataka wasikate tamaa warudi kujipanga upya kwa ajili ya mwakani.

    Yanga juzi ilikubali kipigo cha mabao 3-1 dhidi ya Medeama SC ya Ghana na kupoteza matumaini ya mabingwa hao wa Tanzania kucheza nusu fainali ya michuano hiyo baada ya kuwa na pointi moja katika michezo minne waliyocheza.

    Mayanja amesema kinachowashinda Yanga ni kushindwa kutofautisha mashindano ya Kombe la Shirikisho yana utofauti mkubwa na yale ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara, ndiyo maana wamejikuta wakishindwa kufanya
    vizuri katika mechi zao nne walizocheza.

    “Pamoja na kwamba wana timu nzuri lakini siyo kwenye michuano
    hiyo walichotakiwa ni kufanya mabadiliko kwa kusajili wachezaji wenye uzoefu kwenye sehemu muhimu kama za ulinzi na kiungo,lakini wenyewe baada ya kufanya vizuri kwenye ligi wakakiamini kikosi chao na kwenda nacho kwenye michuano ya CAF, walisahau kwamba huko kuna timu zimejiandaa na zina wachezaji wenye uwezo mkubwa,” alisema Mayanja.

    Kocha huyo alisema matokeo waliyoyapata Yanga kwenye michuano hiyo yanapaswa yachukuliwe kama somo kwa kukirekebisha kikosi chao ili mwakani waweze kufanya vizuri kwa sababu bado watashiriki tena michuano hiyo kutokana na ubingwa walioutwaa msimu uliopita.

    Alisema ugumu uliopo kwenye mashindano hayo alijua wazi kama Yanga wangekuwa washiriki
    kutokana na udhaifu wa kikosi walichokuwa nacho ambacho ushindani wake upo kwenye ligi ya ndani pekee na siyo kwenye michuano hiyo mikubwa Afrika.

    Mayanja alisema Yanga wasitafute mchawi kwa sababu matokeo wanayoyapata hivi sasa walistahili kulingana na ubora wa timu waliyokuwa nayo na kuwatahadharisha wasipoangalia hali hiyo inaweza kuendelea kuwakuta hadi kwenye msimu mpya wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara inayotarajia kuanza Agosti 20.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: KOCHA SIMBA AIPA POLE YANGA,AELEZA KILICHOIUA SHIRIKISHO Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top