Morogoro,Tanzania.
KLABU ya Simba SC imeanza vyema kampeni zake za kujiwinda na msimu mpya wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya jioni ya leo kuichapa Polisi Morogoro kwa jumla ya mabao. 6-0 katika mchezo Mkali wa kirafiki uliochezwa jioni ya leo mjini Morogoro.
Mabao yaliyoipa Simba SC ushindi huo mnono yamefungwa na Mshambuliaji toka Ivory Coast, Frederick Blagnon aliyefunga mabao mawili sawa na Mtanzania,Ibrahim Hajib,huku Abdi Banda na Mohammed Mussa wakifunga bao moja kila mmoja.
Kikosi cha Simba SC kilikuwa:
Vincent Angban, Janvier Besala Bokungu/Hamad,Mohammed Hussein ‘Tshabalala’/Abdi Banda, Method Mwanjali, Novat Lufunga/Juuko Murushid,Muzamil Yassin, Mohammed ‘Mo’ Ibrahim/Said Ndemla,Shizza Kichuya/Mohammed Mussa,Frederick
Blagnon/Mussa Mgosi,Peter Mwalyanzi,Ibrahim Hajib/Awadh Juma na Jamal Mnyate/Danny Lyanga.
0 comments:
Post a Comment