London, England.
KOCHA wa zamani wa Sunderland,Sam Allardyce,ametangazwa kuwa kocha mpya wa timu ya taifa ya England akichukua nafasi iliyoachwa wazi na Roy Hodgson aliyejiuzulu baada ya kung'olewa mapema katika michuano ya Euro 2016.
Allardyce,61,maarufu kama Big Sam amepata nafasi hiyo baada ya kuwabwaga waliokuwa wapinzani wake katika kinyang'anyiro hicho, Makocha Steve Bruce na Jurgen Klinsmann.
Kibarua cha kwanza cha Allardyce kitakuwa Septemba 4 pale atakapoiongoza England kuvaana na Slovakia.
0 comments:
Post a Comment