London, England.
BEKI wa Arsenal,Per Mertesacker,anatarajiwa kukaa nje ya dimba kwa kipindi cha miezi mitano baada ya kupata jeraha la goti
Mertesacker,31,alipata jeraha hilo Ijumaa iliyopita wakati akiichezea Arsenal katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya RC Lens ya Ufaransa ulioisha kwa sare ya bao 1-1.
Kuumia kwa Mertesacker ni pigo kwa kocha wa Arsenal Mfaransa,Arsene Wenger,ambaye hivi karibuni alitarajia kumtangaza beki huyo wa zamani wa Weder Bremen kuwa nahodha mpya wa klabu hiyo kufuatia kuondoka kwa Mhispania,Mikel Arteta aliyejiunga na benchi la ufundi la Manchester City.
Wakati huohuo,Mertesacker,ameachwa katika kikosi cha Arsenal kilichosafiri Jana mchana kwenda Marekani kucheza michezo ya kimataifa ya kujipima nguvu.
0 comments:
Post a Comment