728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, July 21, 2016

    ALIYETUPIWA VIRAGO FC PORTO ATANGAZWA KOCHA MKUU TIMU YA TAIFA YA HISPANIA

    Madrid,Hispania.

    Julian Lopetegui,49, ametangazwa kuwa Kocha Mkuu Mpya wa timu ya taifa ya Hispania akichukua mikoba ya Vicente del Bosque aliyemaliza kandarasi yake hii ikiwa ni miezi sita tu tangu atupiwe virago na FC Porto.

    Kabla ya kupewa jukumu hilo kubwa,Lopetegui aliwahi kuvinoa vikosi vya vijana vya Hispania vya chini ya umri wa 19,20 na 21 na kufanikiwa kushinda vikombe viwili vya Ulaya vya chini ya umri miaka 19 na 21 pia aliwahi kuichezea Hispania katika fainali za kombe la dunia la mwaka 1994 lililofanyika nchini Marekani.

    Lopetegui alianza kazi ya ukocha mwaka 2003 kabla ya hapo aliwahi kuvichezea vilabu vya Real Madrid, Logroñés, Barcelona na Rayo Vallecano na anatarajiwa kuanza kibarua cha kuinoa Hispania mwezi Septemba pale itakapovaana na Ubelgiji katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: ALIYETUPIWA VIRAGO FC PORTO ATANGAZWA KOCHA MKUU TIMU YA TAIFA YA HISPANIA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top