Celtic, Scotland.
MABINGWA wa Ligi Kuu England,Leceister City usiku huu wamechomoza na ushindi wa penati 6 dhidi ya 5 za Celtic katika mchezo Mkali wa kimataifa wa Kirafiki wa michuano ya International Champions Cup uliochezwa katika Uwanja wa Celtic Park huko Glasgow, Scotland.
Mpaka dakika tisini zinaishi matokeo yalikuwa sare ya bao 1-1.Leceister City ndiyo waliotangulia kupata bao dakika ya 46 kupitia kwa Riyad Mahrez kabla ya Celtic kusawazisha dakika ya 59 kupitia kwa Eoghan
O’Connell.
Penati za Leceister City zimefungwa na Danny Drinkwater,Ben Chilwell,Daniel Amartey,Shinji Okazaki,Marcin Wasilewski na Christian Fuchs huku zile za Celtic zikifungwa na Ryan Christie,Scott Allan,Stefan Johansen,Nadir Ciftci.Penati ya James Forrest ilidakwa na kipa wa Leceister City.
0 comments:
Post a Comment