Kalidou Koulibaly
London,England.
KOCHA Mpya wa Chelsea,Muitaliano Antonio Conte anataka kuiona klabu yake ikiwa moto wa kuotea mbali msimu ujao na katika kuhakikisha hilo linafanikiwa tayari ameutaka uongozi wa klabu hiyo kusajili wachezaji wengine wanne wapya katika kipindi hiki cha usajili barani Ulaya.
Kwa mujibu wa ripoti kutoka,The Daily Mail,ni kwamba tayari Conte,46, ameshazungumza na mabosi wa Chelsea,Roman Abramovich,Marina Granovskaia,Michael Emenalo na kuwaeleza kuwa anataka kusajili wachezaji wengine wanne wapya kabla ya kucheza mchezo wake wa kwanza wa ligi kuu England dhidi ya West Ham katika uwanja wa Stamford Blidge.
Wachezaji anaowataka Conte ni pamoja na mshambuliaji mmoja mwenye hadhi ya dunia (World Class Striker),Mabeki wawili na Kipa mmoja wa kuwapa changamoto Makipa waliopo katika kikosi cha sasa.
Majina yanaohusishwa kuwa katika orodha yake ya matamanio (Wish list) ni pamoja na washambuliaji Alvaro Morata wa Real Madrid na Romelu Lukaku wa Everton.Mabeki ni Kalidou Koulibaly wa Napoli,Victor Lindelof wa Benfica, Kostas Manolas wa AS Roma na Leonardo Bonucci wa Juventus,Kipa wa AC Milan,Diego Lopez.
Mpaka sasa Chelsea imeshafanikiwa kusajili wachezaji wawili.Wachezaji hao ni Michy Batshuayi aliyetokea Marseille na N’Golo Kante aliyetoka Leceister City.
0 comments:
Post a Comment