Zanzibar
NYOTA wa timu ya Caps United ya Zimbabwe, Brian Abbas Amidu,ametua visiwani Zanzibar leo mchana tayari kabisa kuanza majaribio ya kujiunga na Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC.
Amidu aliyetua nchini jana akitokea Zimbabwe, mara baada ya kutua visiwani hapa alianza moja kwa moja mazoezi na wenzake wakati wakifanya programu maalumu ya kunyoosha
viungo kwenye bwawa la kuogelea ndani ya Hoteli ya Kitalii ya Mtoni Marine ilipofikia Azam FC.
Mshambuliaji huyo, 26,mwenye uwezo
pia wa kucheza kama kiungo mshambuliaji hakuwa na maneno
mengi ya kusema mara baada ya kuwasili bali ameweka wazi kuwa yupo
tayari kupambana na kuonyesha kipaji chake ili hatimaye aweze kufuzu na
kusajiliwa.
Amidu anaungana na nyota mwingine wa Kimataifa wa Zimbabwe, Bruce Kangwa, ambaye bado anaendelea na majaribio yake akiwa ametimiza wiki moja hivi leo.
Mbali na kucheza katika kikosi cha Caps United, Amidu amefanikiwa kucheza soka la kulipwa kwa miaka minne kabla ya Januari mwaka huu kurejea nyumbani na kujiunga na
Caps.
Usajili wake wa kwanza kucheza kimataifa ilikuwa ni mwaka 2012 alipojiunga na Kaizer Chiefs ya Afrika
Kusini kasha akapelekwa Black Leopards ya huko kabla ya Machi mwaka jana kutua Masafi SC inayoshiriki Ligi Kuu ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE).
Wachezaji wengine waliokuwa kwenye
majaribio Azam FC ni washambuliaji Ibrahima Fofana (Ivory Coast) anayeweza pia kucheza kama winga wa kushoto pamoja na Mrundi Fuadi
Ndayisenga.
0 comments:
Post a Comment