Madrid,Hispania.
KEVIN GAMEIRO amejiunga na klabu ya Atletico Madrid kwa mkataba wa miaka minne akitokea klabu ya Sevilla kwa ada ya awali ya €32m ambayo itapanda na kufikia €37m.
Atletico Madrid imemua kumsajili Gameiro,29,baada ya kocha wake Mkuu,Muargentina Diego Simeone,kuitaka bodi ya klabu hiyo kusajili mshambuliaji mwingine mkali ambaye atasaidiana na Antoine Griezmann ili kuiletea mataji klabu hiyo ya Vicente Cardelon.
Msimu uliopita Gameiro aliifungia Sevilla mabao 29 na kuiwezesha kutwaa ubingwa wa Europa Ligi baada ya kuifungia bao moja katika ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Liverpool katika mchezo wa fainali uliochezwa Mwezi Mei huko Basel,Uswisi
Gameiro anakuwa mchezaji wa tano kujiunga na Atletico Madrid tangu dirisha la usajili barani Ulaya lilipofunguliwa rasmi mwezi uliopita.Wengine ni Nico Gaitan, Sime Vrsaljko, Diogo Jota na Axel Werner.
Gameiro anaiacha Sevilla akiwa ameifungia jumla ya mabao 67 na kuisaidia kutwaa mataji matatu ya Europa Ligi katika kipindi cha miaka mitatu alichoichezea klabu hiyo ya Ramon Sanchez Pizjuan.
Kabla ya kutua Sevilla,Gameiro,aliwahi kuvichezea vilabu vya nyumbani kwao Ufaransa vya Lorient na Paris Saint-Germain.
0 comments:
Post a Comment