Turin,Italia.
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Argentina,Gonzalo Higuaín,amejiunga na mabingwa wa Italia,Juventus,akitokea Napoli pia ya Italia kwa ada ya uhamisho ya £75.3m (€94m) ambayo ni kubwa zaidi kuwahi kutolewa kwa mchezaji nchini humo.
Higuaín,28,amesaini mkataba wa miaka minne wa kuitumikia miamba hiyo ya jiji la Turin baada ya kufaulu vipimo vyake vya afya alivyofanyiwa Ijumaa iliyopita.
Mkataba huo wa miaka minne utamfanya Higuain awe akilipwa mshahara wa £6.3m kwa mwaka na kuwa mchezaji wa tatu duniani kuwahi kusajiliwa kwa ada kubwa nyuma ya Gareth Bale na Cristiano Ronaldo.
Higuain anakuwa mchezaji wa tano kujiunga na Juventus baada ya Miralem Pjanic, Dani Alves, Marko Pjaca, Mario Lemina na Medhi Benatia.
Akiwa na Napoli msimu uliopita Higuain alifanikiwa kufunga mabao 36 katika michezo 35 hali iliyofanya vilabu vingi vya Ulaya vianze kumtolea macho lakini ni Juventus pekee ndiyo iliyoonyesha nia ya kweli ya kuitaka huduma yake.
0 comments:
Post a Comment