Lens,Ufaransa.
ARSENAL imekwepa kichapo katika mchezo wake wa kwanza wa maandalizi ya msimu mpya baada ya kulazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na RC Lens katika mchezo mkali wa kimataifa wa kirafiki uliochezwa usiku huu katika uwanja wa Stade Bollaert-Delelis jijini Lens,Ufaransa.
Wenyeji RC Lens ndiyo waliokuwa wa kwanza kupata bao la kuongoza baada ya Mathias Autret kufunga dakika ya 37 ya mchezo akitumia makosa ya mlinzi Calum Chambers aliyeshindwa kuondosha vyema mpira langoni mwake.
Kuingia kwa bao hilo kuliiamsha Arsenal ambayo ilikuja juu na kufanikiwa kupata bao la kusawazisha dakika ya 82 kupitia kwa winga wake,Alex
Oxlade-Chamberlain.
Arsenal itacheza mchezo wake wa pili wa kujipima nguvu Julai 29 pale itakapovaana na kombaini ya Marekani huko San Jose.
Kikosi cha Arsenal kilikuwa hivi:
Arsenal: Martinez, Debuchy,
Mertesacker, Chambers, Monreal,Elneny, Coquelin, Walcott, Iwobi, Reine-
Adelaide, Akpom
Akiba:Macey, Gibbs, Bielik,Zelalem, Campbell, Oxlade-Chamerlain,Willock, Gnabry
0 comments:
Post a Comment