Dar es Salaam,Tanzania.
KAMPUNI ya Bia Tanzania (TBL) imeamua kutosaini mkataba wa kuendelea kuidhamini Simba.
Taarifa kutoka ndani ya Simba, zinaeleza TBL imegoma kusaini mkataba
ikionekana kuingia hofu baada ya Yanga kutotaka kuendelea nao au waingie
wakiwa na ofa mpya.
Pamoja na hiyo imeelezwa kumekuwa na juhudi binafsi zinazofanywa na
baadhi ya viongozi kujaribu kuwashawishi TBL kupitia Kilimanjaro,
wabadili uamuzi.
Hata hivyo, Katibu Mkuu wa Simba, Patrick Kahemele alisema jana
mkataba huo na TBL unamalizika mwishoni mwa mwezi ujao na Simba haina
mpango wa kuongeza tena.
Kahemele alisema kuwa makampuni kibao makubwa hapa nchini yanagombea
kuingia mkataba na Simba na klabu hiyo inatafakari nani wa kuingia naye
mkataba kutokana na fungu kubwa la fedha.
Alisema Simba ni timu kubwa na makampuni mengi yanataka kuingia nayo
mkataba, hivyo ule wa TBL ulikuwa mdogo na unamalizika mwishoni mwa
mwezi ujao.
Alisema baada ya kumalizika kwa mkataba huo, Simba itatangaza makampuni yanayotaka kufanya biashara na Simba.
0 comments:
Post a Comment