728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, July 30, 2016

    PIGO:NYOTA MPYA LIVERPOOL NJE MIEZI MIWILI BAADA YA KUVUNJIKA MFUPA WA MKONO

    California, Marekani.

    ILE kiu ya Mashabiki wa Liverpool kumuona kipa wao mpya,Loris Karius,akianza katika kikosi cha kwanza cha klabu hiyo imekatika ghafla baada ya kipa huyo aliyetarajiwa kuwa chaguo la kwanza kuvunjia mfupa wa mkono.

    Karius,23,alipata jeraha hilo Jumatano Alfajiri huko Pasadena/California nchini Marekani wakati akiichezea Liverpool katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Chelsea baada ya kugongana na beki wake Dejan Lovren wakati akijaribu kuokoa mpira wa faulo uliopigwa na Willian.

    Taarifa iliyotufikia hivi punde imesema baada ya kufanyiwa vipimo vya kina imebainika kuwa Karius amevunjika mfupa mmoja wa mkono wake wa kulia na atakuwa nje ya dimba kwa kipindi cha miezi miwili kwani jeraha hilo linahitaji upasuaji ili liweze kupona vizuri.

    Hii ina maana kwamba sasa Liverpool italazimika kuhamishia matumaini yake kwa kipa asiye na ushawishi mkubwa klabuni hapo Mbelgiji,Simon Mignolet mpaka hapo Karius atakapokuwa amepona kabisa na kurejea dimbani.

    Karius alijiunga na Liverpool mwezi Juni mwaka huu akitokea Mainz 05 kwa ada ya £4.7m

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: PIGO:NYOTA MPYA LIVERPOOL NJE MIEZI MIWILI BAADA YA KUVUNJIKA MFUPA WA MKONO Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top