728x90 AdSpace

Thursday, July 28, 2016

REAL MADRID HOI ICC YACHAPWA 3-1 NA PSG

Ohio,Marekani.

REAL MADRID imeanza vibaya maandalizi ya msimu mpya baada ya Alfajiri ya leo kufungwa mabao 3-1 na Paris Saint Germain katika mchezo mkali wa kimataifa wa kirafiki wa michuano ya International Champions Cup (ICC) uliochezwa katika uwanja wa Ohio Stadium huko Columbus,Marekani.

Mabao yaliyoipa Paris Saint Germain ushindi yamefungwa na kinda Jonathan Ikone dakika ya 2 huku mlinzi mpya wa klabu hiyo Mbelgiji Thomas Meunier akifunga mara mbili dakika za 35' na 40'.Bao la Real Madrid limefungwa kwa mkwaju wa penati na mlinzi wake wa kushoto,Marcelo.

Katika mchezo huo Real Madrid iliwakosa nyota wake Cristiano Ronaldo, Gareth Bale na Sergio Ramos ambao bado wako mapumzikoni.Paris Saint Germain iliwakosa Marco Verratti, David Luiz na Grzegorz Krychowiak,

VIKOSI

PARIS SAINT-GERMAIN XI: Trapp,Aurier, Thiago Silva, Kimpembe, Kurzawa,Callegari, Rabiot, Pastore, Lucas, Ikone,Cavani

REAL MADRID XI: Casilla, Varane,Nacho, Marcelo, Casemiro, Kovacic, Lucas
Vasquez, Jese, Morata, Isco, Danilo

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Post a Comment

Item Reviewed: REAL MADRID HOI ICC YACHAPWA 3-1 NA PSG Rating: 5 Reviewed By: Unknown