Beijing, China.
ILE hamu ya mashabiki wa vilabu vya Manchester United na Manchester City kuona vilabu vyao vikipepetana leo mchana katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki wa michuano ya ICC imeingia nyongo baada ya pambano hilo kufutwa kutokana na hali mbaya ya hewa kulikumba jiji la Beijing ambalo lilipangwa kuwa mwenyeji wa mpambano huo.
Taarifa kutoka Beijing,China zinasema uamuzi huo umefikiwa baada ya waandaaji wa michuano hiyo pamoja na wakuu wa vilabu hivyo viwili kufikia makubaliano kuwa mchezo huo ufutwe baada ya mvua zinazoendelea kunyesha jijini humo kuharibu miundombinu ya uwanja hali ambayo inatishia afya za machezaji ikiwemo kupata majeraha.
0 comments:
Post a Comment