Riyad Mahrez.
Gundogan:Kiungo wa zamani wa Manchester United,Paul Scholes,ameutaja usajili wa kiungo wa Ujerumani,Ilkay Gundogan,kwenda Manchester City kuwa ndiyo usajili bora zaidi kwasasa ligi kuu England.(MEN)
Mahrez:Meneja wa Leicester City,Muitaliano Claudio Ranieri,kwa mara nyingine tena amesisitiza kuwa winga wa klabu hiyo,Mualgeria Riyad Mahrez,hataihama klabu hiyo licha ya kuwepo kwa taarifa kuwa anatakiwa na Arsenal kwa dau la £41.8m.
Lukaku:Chelsea italazimika kutoa kitita cha £75m ili kuishawishi Everton ikubali kumuuza mshambuliaji wake Mbelgiji,Romelu Lukaku,23.(Daily Mail)
Kroos:Meneja wa Manchester City,Pep
Guardiola,anafikiria kuachana na mpango wa kutaka kumsajili kiungo wa Real Madrid,Toni Kroos, mwenye thamani ya £60m baada ya kutishwa na ukubwa wa mshahara anaoutaka nyota huyo wa zamani wa Bayern Munich. (The Sun)
Meyer:Liverpool imeripotiwa kuwa tayari kutoa kitita cha £28m ili kuinasa saini ya kiungo wa Schalke,Mjerumani Max Meyer.(Bild)
Lacazette:Arsenal imeripotiwa kutenga kitita cha £75m ili kuwasajili winga wa Leceister City,Riyad Mahrez, na mshambuliaji wa Olympique de Lyon,
Alexandre Lacazette.
Ginter:Borussia Dortmund imeitaka Arsenal kuachana kabisa na mpango wa kutaka kumsajili beki wake wa kati,Matthias Ginter,kwani nyota huyo mwenye miaka 23 hauzwi.(Daily Star)
Bacca:Napoli imeripotiwa kuwa inafikiria kusajili mshambuliaji mmoja kati ya Alexandre Lacazette wa Lyon ama Carlos Bacca wa AC Milan ili kuchukua nafasi ya mshambuliaji wake Gonzalo Higuain anayekaribia kujiunga na Juventus.(Inside Football)
Witsel:Muda wowote kuanzia sasa Everton huenda ikafanikiwa kumsajili kiungo wa Ubelgiji,Axel Witsel (27),hii ni baada ya ofa yake ya £25.1 kukubaliwa na klabu yake ya Zenit St Petersberg ya Urusi.(The Sun).
Smith:Liverpool imekubali ofa ya £6.5m kutoka Bournemouth kwa ajili ya kumuuza beki wake wa kushoto raia wa Australia,Brad Smith.Taarifa zaidi zinasema tayari Liverpool imeshatoa ruhusa kwa Smith,22,kwenda kufanyiwa vipimo vya afya.(Sky Sports)
De Vrij:Chelsea imekata tamaa kumnasa beki wa kati wa Napoli,Kalidou Koulibaly,na sasa imeelekeza nguvu zake kujaribu kumsajili beki wa Lazio,Stefan de Vrij,ambaye anapatikana kwa dau dogo la £15m.(Daily Mirror)
Mascherano:Juventus imeripotiwa kuwa itatumia sehemu ya pesa itakayopata katika mauzo ya kiungo wake Mfaransa Paul Pogba,23,kwenda Manchester United ili kumsajili kiungo wa Barcelona Muargentina,Javier Mascherano,32.(Gazzetta dello Sport)
0 comments:
Post a Comment