Stoke,England.
WINGA wa Kimataifa wa Misri,Ramadan Sobhi,amejiunga na Stoke City akitokea Al Ahly kwa ada ya £5m.
Sobhi,19,mwenye uwezo wa kucheza winga ya kushoto,kulia na namba 10 amejiunga na Stoke City maarufu kama The Potters (Wabeba Mizigo) baada ya mazungumzo yaliyochukua miezi miwili.
Sobhi anakuwa mchezaji wa kwanza wa Misri kujiunga na Stoke City pia anakuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na klabu hiyo katika kipindi hiki cha usajili barani Ulaya.
Akiwa na Al Ahly,Sobhi,alifanikiwa kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya Misri mara mbili mwaka 2014 na 2016 pamoja na ubingwa wa Super cup mwaka 2014 na 2015.
0 comments:
Post a Comment