728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, July 22, 2016

    ARSENAL DIMBANI LEO INACHEZA MCHEZO WAKE WA KWANZA WA KUJIPIMA NGUVU

    Lens,Ufaransa.

    ARSENAL leo itaanza kucheza michezo yake ya kujipima nguvu tayari kwa Msimu Mpya wa Ligi Kuu England na Michuano mingine pale itakaposhuka katika dimba la Stade Bollaert-Delelis lililoko Lens,Ufaransa kuvaana na Wenyeji wao RC Lens. 

    Katika Mchezo huo unaotarajiwa kuwa utatoa picha ya kile wachezaji wa timu hizo mbili wamekipata baada ya kuwa katika mazoezi ya zaidi ya wiki moja,Arsenal itawakosa nyota wake wanane wa kikosi cha wakubwa kufuatia kuwa katika Mapumziko ya wiki nne baada ya kutoka kuzitumikia timu zao za taifa katika michuano ya Copa America na Euro 2016.

    Nyota hao ni Alexis Sanchez, Laurent Koscielny, Olivier Giroud,Mesut Ozil,Aaron Ramsey,Peter Cech na David Ospina.

    Baada ya Mchezo huo Arsenal itasafiri mpaka Marekani ambapo itacheza mchezo mwingine wa kujipima nguvu Julai 28 huko San Jose kwa kuvaana na Kombaini ya Marekani maarufu kama MLS All-Stars ambayo itakuwa na nyota kama Didier Drogba,David Villa,Andre Pirlo na Ricardo Kaka.

    Kikosa cha Arsenal leo huenda kikawa hivi.Mchezo utachezwa saa tatu usiku.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: ARSENAL DIMBANI LEO INACHEZA MCHEZO WAKE WA KWANZA WA KUJIPIMA NGUVU Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top