Marseille,Ufaransa.
MSHAMBULIAJI mahiri wa Swansea City,Bafetimbi Gomis,ameihama klabu hiyo na kujiunga na klabu ya Marseille ya nyumbani kwao Ufaransa kwa mkopo wa msimu mmoja.
Gomis,30,amejiunga na Marseille baada ya klabu hiyo kukubali kulipa asilimia 60% ya mshshara wake huku Swansea City inayommiliki ikilipa asilimia 40.
Taarifa zaidi zimasema Gomis ameamua kuihama Swansea City baada ya kutopata namba mara kwa mara katika kikosi cha kocha Muitaliano Francesco Guidolin.
Tangu Guidolin apewe mikoba ya kuinoa Swansea City mwezi Januari,Gomis alijikuta akipoteza namba kwani mpaka ligi inaisha mwezi Mei alifanikiwa kuanza katika kikosi cha kwanza katika michezo mitatu pekee.
Gomis anakuwa mshambuliaji wa tatu kuihama Swansea City katika kipindi hiki cha usajili barani Ulaya.Wengine ni Alberto Paloschi na Eder ambaye bao lake liliipa Ureno ubingwa wa Euro 2016 nchini Ufaransa.
Mwanzoni mwa msimu uliopita Gomis alijizolea umaarufu mkubwa baada ya kuvifunga mabao murua vilabu vya Manchester United,Arsenal na Chelsea huku staili yake ya ushangiliaji inayofanana na mwendo wa dubu/simba ikigeuka kivutio zaidi.
0 comments:
Post a Comment