Villarreal,Hispania.
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Brazil,Alexandre Pato,amejiunga na klabu ya Villarreal ya Hispania akitokea klabu ya Corinthians kwa mkataba wa miaka minne.
Pato,26,amejiunga na Villarreal kwa ada inayodhaniwa kufikia €3m.Pia katika uhamisho huo itashuhudiwa Villarreal ikimmiliki Pato kwa asilimia 60 pekee huku asilimia 40 zilizobaki zikimilikiwa na nyota huyo wa zamani wa AC Milan.
Pato amejiunga na Villarreal baada ya kushindwa kupata mafanikio katika kikosi cha Chelsea alichokichezea kwa mkopo msimu uliopita ambapo alifanikiwa kufunga bao moja pekee.
0 comments:
Post a Comment