728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, July 23, 2016

    RIYAD MAHREZ AKUBALI KUTUA ARSENAL KWA €50M

    London,England.

    WINGA wa Leceister City na mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa Ligi Kuu ya England,Mualgeria Riyad Mahrez,amekubali kujiunga na Arsenal.

    Taarifa kutoka nchini Ufaransa na kuchapishwa na mtandao wa French Eurosport zinasema wakala wa Mahrez alikutana na mabosi wa Arsenal jana Ijumaa usiku na kufikia makubaliano hayo ya mteja wake kuhamia Emirates kwa ada ya €50 (£41.8m).Jana Arsenal ilikuwa Ufaransa ikicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Lens.

    Kinachosubiriwa sasa ni vilabu vya Arsenal na Leceister City kukaa mezani na kukamilisha dili hilo.

    Msimu uliopita Mahrez alifunga mabao 17 na kutengeneza mengine 11 ambayo ni idadi kubwa kuliko mchezaji yoyote yule wa Arsenal.

    Mahrez alijiunga na Leicester City mwaka 2014 akitokea Le Havre ya Ufaransa kwa ada ya £400,000 na amebakiza miaka mitatu katika mkataba wake na klabu ya Leceister City.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: RIYAD MAHREZ AKUBALI KUTUA ARSENAL KWA €50M Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top