Genk,Ubelgiji.
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta,amefunga bao na kuiwezesha klabu yake ya KRC Genk kuchomoza kifua mbele kwa ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya KV Oostende katika mchezo mkali wa ligi kuu ya Ubelgiji ulioisha hivi punde katika uwanja wa Cristal Arena jijini Genk.
Mabao ya KRC Genk katika mchezo huo yametiwa kimiani dakika za 49 na 90 kupitia kwa Nikolaos Karelis na Mbwana Ally Samatta aliyekuwa ameingia uwanjani dakika ya 80 kuchukua nafasi ya Neeskens Kebano.
Bao la kufutia machozi la KV Oostende limefungwa dakika ya 93 na Knowledge Musona.
Vikosi
KRC Genk:Bizot, Walsh, Dewaest, Karelis,Wouters, Buffels Uronen, Pozuelo (82' Heynen), Ndidi, Bailey (71'
Trossard), Kebano (79' Samatta)
KV Oostende:Proto, Antunes, Siani, El Ghanassy (63' Marusic), Musona, Dimata (63 'Cyriac) , Jonckheere, Capon,
Tomasevic, Milic, Canesin (79' Akpala)
0 comments:
Post a Comment