Los Angels,Marekani.
ARSENAL imehitimisha vyema ziara yake ya michezo ya kujipima nguvu nchini Marekani baada ya usiku wa kuamkia leo kuibuka na ushindi murua wa mabao 3-1 dhidi ya Chivas de Guadalajara ya Mexico katika mchezo mkali wa kimataifa wa kirafiki uliochezwa katika uwanja wa StubHub Centre ulioko Los Angles,Marekani.
Arsenal ilianza kujihakikishia ushindi mapema tu dakika ya (33) ya mchezo baada ya beki wake mpya Rob Holding kufunga bao la kuongoza lililofuatiwa na mabao mengine kutoka kwa Alex Oxlade-Chamberlain (50') na Chupa Akpom (56').
Dakika ya 74 Angel Zaldivar aliifungia Chivas de Guadalajara bao la kufuatia machozi kwa mkwaju wa penati baada ya beki wa kulia wa Arsenal,Mathieu Debuchy,kumfanyia madhambi Luis Zendejas ndani ya boksi.
Vikosi
Arsenal: Ospina, Bellerin, Chambers, Holding,Monreal, Xhaka, Coquelin, Oxlade-Chamberlain, Cazorla, Iwobi, Walcott
Chivas: RodrÃguez; Villanueva, Basulto,
AlanÃs, 'Pocho'; Lázaro, OrbelÃn, Torres,
'Chofis'; González y BenÃtez
0 comments:
Post a Comment