Manchester, England.
KIUNGO wa zamani wa England na Manchester United,Paul Scholes,amesema kiungo wa Ufaransa na Juventus,Paul Pogba,hana thamani ya £86m kama inavyoripotiwa.
Kauli hiyo ya Scholes imekuja baada ya kuwepo kwa taarifa kuwa Manchester United iko katika mazungumzo ya kutaka kumsajili Pogba kwa dau la £86m ikiwa ni miaka minne tangu imuachie ajiunge na Juventus kwa uhamisho huru.
Akifanya mahojiano na Sport Witness,Scholes, amekataa katakata kukubaliana na dau hilo ambalo Manchester United imeripotiwa kutaka kulitoa ili kumnasa Pogba kwa mara ya pili.
Scholes amekiri kwamba Pogba ni mchezaji mzuri,anamjua,amecheza nae lakini amesisitiza dau la £86m siyo saizi yake na kuongeza kuwa dau hilo ni la kuwanunua watu ambao wanaweza kufunga mabao 50 kwa msimu mmoja kama wanavyofanya
Ronaldo na Messi na siyo vinginevyo.
Scholes amemaliza kwa kusema Pogba anahitaji kufanya kazi kwa bidii sana kama kweli anataka kufikia kuwa na thamani ya £86m lakini kwasasa thamani hiyo hana.
0 comments:
Post a Comment