Mbeya,Tanzania.
KLABU ya MBEYA City yenye Makao yake Makuu jijini Mbeya imetangaza kumsajili kwa Mkataba wa Miaka miwili Kiungo Fundi, Ayoub Idrisa Semtawa kutoka Klabu ya Coastal Union ya jijini Tanga.
Mbeya City imeamua kumsajili Ayoub Idrisa Semtawa baada ya kukoshwa na kiwango kizuri alichokionyesha msimu uliopita katika michezo ya ligi kuu bara na ile ya shirikisho maarufu kama kombe la Azam FA Cup.
Ayoub anakuwa mchezaji
wa pili kujiunga na Mbeya
City katika kipindi kisichozidi wiki moja,hii ni baada ya mapema wiki hii
Mbeya City kumsajiliwa beki wa Yanga,Rajab Zahir aliyekuwa anacheza kwa mkopo Stand United.fbbm
0 comments:
Post a Comment