Podgorica
KLABU ya KRC Genk inayochezewa na Mshambuliaji wa Kimataifa wa Tanzania,Mbwana Samatta,imefanikiwa kutinga hatua ya pili ya Michuano ya Europa Ligi baada ya Alhamis Usiku kuifunga Buducnost
Podgorica kwa penati 4-2 katika mchezo Mkali wa Marudiano uliochezwa katika Uwanja wa Gradski Podgorica na kuchezeshwa na Mwamuzi,Charalambos Kalogeropoulos,kutoka Ugiriki.
Mchezo huo ulilazimika kufikia hatua ya penati baada ya wenyeji Buducnost Podgorica kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 ya Radomir Djalovic (2) pamoja na Milos Raickovic (40) na kufanya matokeo kuwa sare ya 2-2 kwani Katika Mchezo wa Kwanza uliochezwa huko Genk katika Uwanja wa Cristal Arena,KRC Genk wakiwa wenyeji walipata ushindi kama huo.
Penati za ushindi wa Genk zimepigwa na Thomas Buffel, Bryan Heynen, Mbwana Samatta na Dries Wouters.Hivyo kwa matokeo hayo sasa Genk itacheza hatua ya pili ya Europa League dhidi ya Cork City ya Jamhuri ya Ireland.
0 comments:
Post a Comment