Lubumbashi,Congo.
BAO la mshambuliaji wa kimataifa wa Zimbabwe,Rainford Kalaba,mnamo dakika ya 62 limeiwezesha TP Mazembe kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya MO Bejaia ya Algeria katika mchezo mkali wa kundi A wa Kombe la Shirikisho Afrika uliochezwa jioni ya leo katika uwanja wa Stade de Mazembe,Lubumbashi.
Ushindi huo umeifanya TP Mazembe kufikisha pointi kumi na kuendelea kujikita kileleni mwa msimamo wa kundi A.Nafasi ya pili kwasasa imekaliwa na Medeama yenye pointi tano sawa na Mo Bejaia lakini ina uwiano mzuri wa mabao.Nafasi ya nne imekaliwa na Yanga yenye pointi moja.
0 comments:
Post a Comment