728x90 AdSpace

  • Latest News

      Saturday, July 23, 2016

      KUHUSU KUCHEZA SOKA ULAYA,KOCHA YANGA AWATOLEA UVIVU WACHEZAJI WA KIBONGO

      Dar es Salaam,Tanzania.

      KOCHA Mkuu wa Yanga, Hans Van Pluijm amesema wachezaji wengi wa Tanzania hawako tayari kucheza soka la kulipwa barani Ulaya na nchi
      nyingine zilizopiga hatua katika mchezo wa soka.

      Pluijm alisema akijibu swali la kwamba klabu yao imekuwa ngumu kutoa ruhusa kwa nyota wake kucheza soka la kulipwa Ulaya.

      “Kwanza sijui kuhusu kutakiwa kwa wachezaji wangu kwenye nchi za
      Ulaya. Pili kila mmoja anapaswa kujiuliza kama wako tayari kwa ajili ya soka la kulipwa. Wote tunapenda kuona wachezaji wetu wakifanikiwa,”alisema Pluijm.

      Pluijm alisema kwamba kama kuna kitu cha kubadilisha kwenye soka la
      Tanzania ni mtazamo wa wachezaji na viongozi kuelekea kwenye soka la
      kulipwa, kwani mtazamo huo unamuandaa mchezaji kuwa tayari na soka la kulipwa.

      “Kwa baadhi ya wachezaji ni kama utamaduni wa kushangaza kubadili akili na mtazamo wao. Lakini kama unataka kubadili kitu fulani kwa ujumla kwenye soka la Tanzania basi ni mtazamo wao kuelekea kwenye soka la kulipwa.

       “Kubadili mtazamo wao na kuwafanya wawe na shauku ya kutaka kupata tuzo binafsi, kwa klabu zao na timu ya taifa,” alisema Pluijm.

      Kocha huyo kutoka Uholanzi na aliyeiongoza Yanga kufika hatua ya
      makundi ya mashindano ya Kombe la Shirikisho la Soka la Afrika,alisema kuwa wachezaji wa Tanzania wanatakiwa kuiga mfano waa mshambuliaji Mbwana Samatta ambaye kwa sasa anacheza KRC Genk inayoshiriki Ligi Kuu ya
      Ubelgiji.

      “Juma Mahadhi (mchezaji mpya wa timu hiyo kutoka Coastal Union) ana kipaji cha kumfanya acheze soka la kulipwa siku za usoni, lakini tunapaswa kuwa waangalifu na tunavyomchukulia asilewe sifa. Bado kijana mdogo anayetakiwa kujifunza
      mambo mengi kwenye mchezo wa soka,” alisema Pluijm.

      • Blogger Comments
      • Facebook Comments

      0 comments:

      Post a Comment

      Item Reviewed: KUHUSU KUCHEZA SOKA ULAYA,KOCHA YANGA AWATOLEA UVIVU WACHEZAJI WA KIBONGO Rating: 5 Reviewed By: Unknown