728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, July 28, 2016

    AL AHLY YAPATA USHINDI WA KWANZA LIGI YA MABINGWA AFRIKA,ZESCO UNITED YAKOMAA UGENINI

    Rabat,Morocco.

    Al Ahly ikiwa ugenini huko Rabat nchini Morocco imefanikiwa kushinda mchezo wake wa kwanza baada ya kuchomoza na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya wenyeji wao Wydad Casablanca katika mchezo mkali wa kundi A wa michuano ya klabu bingwa Afrika uliochezwa katika uwanja wa Stade Prince Moulay Abdallah huko Rabat,Morocco.

    Bado pekee la mchezo huo limefungwa dakika ya 46 kwa kichwa na kiungo Rami Rabia.Ushindi huo umeifanya Al Ahly ifikishe pointi nne katika nafasi ya tatu nyuma ya Wydad Casablanca na Zesco United zilizo katika nafasi ya kwanza na ya pili.

    Katika mchezo mwingine wa kundi hilo uliochezwa huko Ivory Coast,Zesco United ya Zambia ikiwa ugenini imefanikiwa kuwabana wenyeji wao ASEC Mimosas na kutoka nao sare ya kufungana bao 1-1.

    Nabi Kone alianza kuifungia Asec Mimosas bao la kuongoza kabla ya Jackson Mwanza kuifungia Zesco United bao la kusawazisha.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: AL AHLY YAPATA USHINDI WA KWANZA LIGI YA MABINGWA AFRIKA,ZESCO UNITED YAKOMAA UGENINI Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top