Gothenburg,Sweden.
ZLATAN IBRAHIMOVIC amefunga bao moja na kuiwezesha Manchester United kuibuka na ushindi wa mabao 5-2 dhidi ya Galatasaray katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliochezwa katika Uwanja wa Ullevi huko Gothenburg,Sweden.
Ibrahimovic alianza kuiandikia bao Manchester United dakika ya 4 tu ya mchezo baada ya kufunga kwa mtindo wa Tiki Taka.
Kuingia kwa bao hilo kuliwaamsha vijana wa Galatasaray ambao walikuja juu na kufanikiwa kupata mabao mawili yaliyofungwa dakika za 22 na 40 na Sinan Gümüs pamoja na Bruma na kufanya mchezo uende mapumziko wakiwa kifua mbele kwa mabao hayo mawili.
Kipindi cha pili Manchester United ilijipata vyema na kuwadhibiti wapinzani wao Galatasaray na kufanikiwa kupata mabao manne kati ya hayo mawili yamefungwa na nahodha Kupitia Wayne Rooney aliyefunga mabao mawili dakika za 55 na 59.Marouane Fellaini dakika ya 62 na Juan Mata dakika ya 75.
Manchester United itarejea tena dimbani wiki ijayo kuvaana na Everton katika mchezo maalumu wa kutoa heshima kwa Wayne Rooney kisha itaelekea Wembley kupepetana na Leceister City katika mchezo wa ngao ya jamii ambao huwa maalumu kwa ajili ya ufunguzi wa ligi kuu England.
0 comments:
Post a Comment