California, Marekani.
IKICHEZA mbele ya watazamaji 25,667,Paris Saint-Germain imehitimisha vyema ziara yake ya mazoezi nchini Marekani baada ya asubuhi ya leo kuwachapa Mabingwa wa England,Leceister City kwa jumla ya mabao 4-0 katika mchezo mkali wa kimataifa wa Kirafiki wa michuano ya International Champions Cup (ICC) uliochezwa katika Uwanja wa StubHub Center huko California.
Mabao ya Paris Saint-Germain katika mchezo huo yamefungwa na Edinson Cavani kwa penati dakika ya 26',Jonathan Ikone dakika ya 45',Lucas Moura dakika ya 64' na Odsonne Edouard dakika ya 90'.
Huo unakuwa ni ushindi wa tatu mkubwa kwa Paris Saint-Germain katika michuano hiyo kwani kabla ya kuivaa Leiceister City iliichapa Inter Milan kwa mabao 3-0 kisha ikaichapa Real Madrid kwa mabao 3-1.
Kwa habari zaidi kuhusu mchezo huu na mengine bofya hapa!! http://www.dailymail.co.uk/sport/article-3716624/Paris-Saint-Germain-4-0-Leicester-City-Premier-League-champions-comfortably-beaten-Unai-Emery-s-Los-Angeles.html
0 comments:
Post a Comment