728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, July 20, 2016

    ALVARO NEGREDO AREJEA TENA EPL

    Marbella,Hispania.

    Klabu iliyopanda daraja la ligi kuu England, Middlesbrough,imemsajili kwa mkopo wa mwaka mmoja mshambuliaji wa zamani wa Manchester City,Mhispania Alvaro Negredo kutoka Valencia ya Hispania.

    Negredo,30,ambaye mwaka 2014 aliifungia Manchester City mabao 23 katika michezo 48 na kuiwezesha kutwaa ubingwa wa ligi kuu amesajili ili kuongeza uzoefu katika safu ya ushambuliaji ya Middlesbrough ambayo imepania kufanya makubwa msimu huu.

    Negredo anakuwa mchezaji wa saba kujiunga na Middlesbrough baada ya Antonio Barragan, Victor Valdes, Viktor Fischer,Bernardo Espinosa, Marten de Roon na Jordan McGhee. 

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: ALVARO NEGREDO AREJEA TENA EPL Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top