Shirikisho
la Soka Tanzania (TFF), limetoa madawati 200 ikiwa ni sehemu ya mapato
ya Ngao ya Hisani utakaochezwa Agosti 17, 2016.
Katika
mechi hiyo, Mabingwa watetezi Yanga wataumana na walioshika nafasi ya
pili, Azam FC. Hata hivyo, haijajulikana kama TFF ina uhakika wa kupata
fedha hizo za madawati kwa uamuzi wake wa kutangaza kutoa hata kabla ya
mechi yenyewe.
TFF
inaunga mkono juhudi za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na
juhudi za Serikali kwa ujumla katika kuhakikisha vijana wa Kitanzania
wanakuwa na mazingira bora ya kupata elimu.
Kadhalika
TFF inamshukuru Katibu Mkuu wa Bunge, Dkt. Thomas Kashililah kwa juhudi
za kuendelezaa mpira wa miguu na kuutumia katika kuliletea Taifa
maendeleo.
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania litaendelea kushirikiana na Ofisi ya Bunge
Sports Club katika kufanikisha mashindano mbalimbali hasa mhezo wa
Hisani kati ya Simba Sports Club na Young African (Wabunge)
utakaofanyika hapo baadaye kwa mujibu wa ratiba na uratibu wa Bunge.
0 comments:
Post a Comment