Buenos Aires, Argentina.
KOCHA na nyota wa zamani wa Argentina,Diego Maradona,amesema anatamani tena kibarua cha kukinoa kikosi hicho kwa mara ya pili na kusisitiza kuwa yuko tayari kuchukua jukumu hilo hata bure kabisa yaani bila ya malipo yoyote yale.
Maradona,55,ameweka wazi azma hiyo leo wakati akifanya mahojiano na kituo cha FOX Sports katika kipindi hiki ambacho Argentina inahaha kusaka Kocha Mpya baada ya Gerardo Tata Martino kubwaga manyanga hivi karibuni kufuatia kushindwa kutwaa ubingwa wa Copa America.
Amesema "Diego Simeone hajataka kuinoa Argentina kwa sababu za kifedha.Kwangu fedha siyo kipaumbele.Niko tayari kuwa Kocha wa Argentina hata bila ya malipo yoyote.
Watu wengi wanadhani mimi ni Kocha ghali.Lakini vipi kuhusu Mourinho?Ancelotti ama Simeone?Sijui nina ughali/gharama kiasi gani ukilinganisha na hawa makocha.
Nimeanza kumiss ukocha zaidi na zaidi.Nimemiss karaha za wachezaji.Nimemiss kugombana na waandishi wa habari"
Maradona aliinoa Argentina kuanzia mwaka 2008 mpaka 2010 kabla ya kubwaga manyanga baada ya kufungwa na Ujerumani mabao 4-0 katika mchezo wa robo fainali wa kombe la dunia huko Afrika Kusini.
Mwaka 2011 Maradona alijiunga na Al Wasl ya Qatar na kutimuliwa mwaka mmoja baadae yaani mwaka 2012.
0 comments:
Post a Comment