Liverpool, England.
Liverpool imefanikiwa kumsajili mlinzi wa kati wa Estonia,Ragnar Klavan,kutoka Augsburg ya Ujerumani kwa ada ya awali ya £ £4.2m.
Klavan,30,anayetumia vyema mguu wa kushoto amesaini kandarasi ya miaka mitatu ya kuitumikia miamba hiyo ya Anfield baada ya kufuzu vipimo vyake vya afya na atakuwa akivalia jezi namba 17 katika kipindi chote atakachokuwa akiichezea Liverpool.
Liverpool imemsajili Klavan ili kuongeza uimara katika safu yake ya ulinzi ambayo imepata pigo baada ya kuwapoteza walinzi wake wawili mahiri Mamadou Sakho and Joe Gomez kutokana na majeraha huku walinzi wake wengine Martin Skrtel na Kolo Toure wakihamia vilabu vingine.
Klavan anakuwa mchezaji wa tano kujiunga na Liverpool tangu dirisha la usajili barani Ulaya lilipofunguliwa.Wengine ni Loris Karius, Sadio Mane, Marko Grujic na Joel Matip.
0 comments:
Post a Comment