728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, July 20, 2016

    AZAM FC DIMBANI LEO ASUBUHI

    Dar es Salaam,Tanzania.

    Wakati Azam FC ikiendelea na programu yake ya maandalizi ya msimu ujao kwa siku ya 12 sasa,leo Jumatano inatarajia kucheza mechi ya pili ya kirafiki dhidi ya Friends Rangers inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza (FDL) itakayofanyika Uwanja wa Azam Complex saa 3.00 asubuhi.

    Jumapili iliyopita Kocha Mkuu wa Azam FC, Zeben Hernandez, aliiongoza timu hiyo kwenye mchezo wake wa kwanza na kwa kuifunga Ashanti United mabao 2-0.

    Azam FC inatarajia kuutumia mchezo huo kukipa makali kikosi chake pamoja na kuwafanyia majaribio nyota wa kigeni waliofika klabuni hapo kwa ajili ya kusaka kusajiliwa.

    Nyota hao ni mshambuliaji raia wa Burundi, Fuadi Ndayisenga, aliyetokea Sofapaka ya Kenya alipofunga mabao nane msimu uliopita.

    Ndayisenga anaungana na wachezaji wengine watatu waliokuwa kwenye majaribio, beki wa timu ya Taifa ya Niger, Mohamed Chicoto na mshambuliaji kutoka huko Mossi Moussa Issa pamoja na Ibrahima Fofana wa Ivory Coast.

    Azam FC itacheza mchezo mwingine wa kirafiki Jumamosi ijayo dhidi ya Halmashauri ya Kinondoni (KMC) kabla ya Jumatatu ijayo kutimkia Zanzibar kwa ajili ya kambi ya kutafuta utulivu kwa wachezaji wakati wakipokea mazoezi ya kiufundi kabla ya kurejea na kufanya maandalizi ya mwisho kabla ya kuvaana na Yanga kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii Agosti 17, mwaka huu

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: AZAM FC DIMBANI LEO ASUBUHI Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top