Dar es Salaam,Tanzania.
Makocha wapya watakaoifundisha Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC msimu ujao, walivyotua nchini leo saa 9 Alasiri wakitokea Hispania, tayari kabisa kwa kuanza maandalizi ya msimu mpya Jumatatu Ijayo Julai 4, mwaka huu.
Wakufunzi hao kutoka Hispania waliopokelewa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba pamoja na Ofisa Habari wa timu hiyo, Jaffar Idd, ni Kocha Mkuu Zeben Hernandez na Msaidizi wake Yeray Romero,Kocha Mkuu wa Viungo Jonas Garcia na Msaidizi wake, Pablo Borges na Kocha wa Makipa Jose Garcia.
0 comments:
Post a Comment