Manchester, England.
MSHAMBULIAJI wa Sweden,Zlatan Ibrahimovic atakuwa akivalia jezi namba nane (8) katika kipindi chote atakachokuwa na klabu yake mpya ya Manchester United.
Ibrahimovic,34,ambaye jana Ijumaa alikamilisha usajili wake wa kujiunga na Manchester United akitokea Paris Saint Germain alitarajiwa kuwa angepewa jezi namba tisa (9) lakini hali imekuwa tofauti na sasa atakuwa akivalia jezi namba nane ambayo imekuwa ikivaliwa na Juan Mata.
Badiliko hilo la namba limeibua maswali mengi kwa mashabiki wa soka ambao wameanza kuhofia huenda Mata akauzwa kwani amekuwa hapikiki chungu kimoja na Kocha José Mourinho.
0 comments:
Post a Comment