728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, July 02, 2016

    SERENGETI BOYS YAUA 6-0 SHELISHELI

    Victoria, Shelisheli.

    Timu ya taifa ya Tanzania ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 Serengeti Boys wameibuka na ushindi wa goli 6-0 dhidi ya Shelisheli katika mchezo uliyochezwa katika uwanja wa Linite mjini Victoria, Shelisheli.

    Mchezo ulianza kwa timu zote kushambuliana lakini Serengeti ilionekana kuutawala mchezo huo kwa asilimia kubwa huku Timu hiyo ambayo ni wawakilishi pekee wa nchi kwenye mashindano ya kimataifa ikipata goli lake la kwanza dakika ya tisa kupitia kwa Ibrahim Abdallah baada ya golikipa kutema shuti lililopigwa na Asadi Ally.

    Serengeti boys ilipata goli la pili lililofungwa na Mohemmed Abdallah dakika ya 43 pale alipoachia shuti kali lililomshinda kipa wa wapinzani wao na kuzama wavuni. 

    Hadi kipindi cha kwanza
    kinamalizika serengeti walikuwa kifua mbele Kwa goli 2 huku wakionekana kuutawala vilivyo mchezo huo wa ugenini.

    Kipindi cha pili kilianza kwa Serengeti boys kuingia kwa kasi ambayo ilizaa matunda dakika ya 50 pale Asad Juma anapoandika goli la 3 baada ya kupiga faulo inayotumbukia moja kwa moja wavuni.

    Wageni hao katika uwanja wa Stade Linite walipata bao la 4 kwa penati dakika ya 61 inayopigwa na Issa Makamba na Asad Juma akaandika bao la tano dakika ya 70 huku Yohana Mkomola akimalizia mvua ya magoli dakika ya 90 Kufuatia matokeo hayo Serengeti Boys sasa watakutana na Afrika Kusini baada ya kusonga mbele katika hatua ya pili kwa jumla ya goli 9-0.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: SERENGETI BOYS YAUA 6-0 SHELISHELI Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top