Dar es Salaam,Tanzania.
Kamati ya maadili imetupilia mbali malalamiko ya TFF dhidi ya Mkuu wa kitengo cha habari cha Yanga SC, Jerry Murro.
Kamati hiyo iliyoketi leo Jumamosi jijini Dar es Salaam,imemkosoa mlalamikaji ambaye ni TFF kuwa hata barua ya kumuita Murro ilikuwa na mapungufu kibao hivyo kamati haikuona sababu ya yeye kuitwa na kuhojiwa.
"Nimewasemehe wote waliotaka kunitesa na kunidhalilisha, naomba TFF tuungane pamoja kwa ajili ya soka la nchi yetu"Alisema Murro baada ya kupata taarifa kuwa yupo huru kuendelea na kazi yake.
Mapema wiki hii TFF ilimlima barua Murro ikimtaka afike mbele ya kamati yake ya maadili kujibu tuhumu za zilizodaiwa kuwa amekuwa akilisema vibaya shirikisho hilo katika vyombo vya habari.
0 comments:
Post a Comment