Dar es salaam,Tanzania.
Klabu ya Simba SC imetangaza rasmi kuwatema washambuliaji wake wawili wa kimataifa Pape Ndaw (Senegal) na Simon Sserunkuma (Uganda).
Simba SC imefikia hatua hiyo baada wachezaji hao kushindwa kuonyesha makali yao tangu waliposajiliwa kwa mamilioni ya shilingi.
Wakati Ndaw na Sserunkuma wakiondoka,Simba SC imetangaza kulipokea ombi la winga wa zamani wa Azam FC Mganda Brian Majwega aliyeomba kufanya mazoezi na klabu hiyo ya Msimbazi katika wakati huu ambapo nyota huyo anasaka timu ya kuchezea.Kwasasa Majwega ni mchezaji huru baada ya kutemwa na Azam FC msimu uliopita.
0 comments:
Post a Comment